August 11, 2017
SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
11-08-2017

              TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Soka ya Simba Jumapili hii ya tarehe 13-8-2017,saa kumi alasiri itashuka kwenye Uwanja mkuu wa Taifa hapa jijini kucheza na Klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye mchezo wa kirafiki. 

Mchezo huo ni muhimu kwa pande zote mbili kujiandaa na Ligi kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu. 

Simba pia tutautumia mchezo huo kuiwinda klabu ya Yanga, ambayo tutacheza nayo August 23 mwaka huu, kwenye mchezo wa kugombea Ngao ya hisani. 

Baada ya mchezo dhidi ya Wakata miwa hao,Simba inatarajiwa kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mawindo hayo muhimu. 

IMETOLEWA NA... 

HAJI S. MANARA

MKUU WA HABARI SIMBA SC 


SIMBA NGUVU MOJA

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV