August 11, 2017
SIMBA SPORTS
DAR ES SALAAM
11-8-2017


           TAARIFA KWA UMMA
___________

Klabu ya Simba inawatangazia Wanachama wake na wadau wa mchezo wa kandanda kote nchini kuwa Mkutano wake mkuu wa kawaida wa kila mwaka upo pale pale. 

Hatua hiyo inafuatia na Hukumu iliyosomwa leo katika Mahakama ya kisutu, kufuatia zuio la kuzuia Mkutano huo, liliowekwa na mmoja wa wadhamini wa klabu Mzee Hamis kilomoni. 

Kwenye hukumu hiyo,mahakama hiyo ilitupilia mbali shauri hilo. 

Mkutano huo utafanyika siku ya Jumapili tarehe 13-8-2017, kuanzia saa Nne kamili asubuhi, ukitanguliwa kwa Wanachama wa klabu kujiandikisha kuanzia saa mbili kamili asubuhi. 

Klabu imeamua kufanyia mkutano huo kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere international Conference Centre). 

Ukumbi huo wa kisasa kabisa nchini upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha(IFM), Na itakuwa mara ya kwanza kwa vilabu vya michezo nchini kufanyia mkutano wake kwenye kituo hicho kilichobeba jina la Baba wa Taifa hili. 

Uongozi wa Simba unawaomba wanachama wake kuhudhuria kwa wingi kwenye mkutano huo muhimu,huku mahitaji yote muhimu yakipatikana siku hiyo ikiwemo Vinywaji baridi na Chakula cha mchana. 

Mwisho

klabu inawaomba tena Wanachama wake wenye hoja tofauti waje kuzitoa ndani ya Mkutano huo kama inavyoagiza katiba ya klabu. 

Hakika huu ni ushindi mkubwa sio tu kwa klabu, bali kwa Mustakbali mzima wa maendeleo ya mchezo huu murua zaid nchini na kote Ulimwenguni. 

IMETOLEWA NA.. 

HAJI S MANARA

MKUU WA HABARI SIMBA SC 


SIMBA NGUVU MOJA

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV