August 11, 2017Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amefukuzwa mjini Dodoma na kurejeshwa Dar es Salaam kwa kosa la kumsalimia Mgombea wa Urais wa TFF, Shija Richard.

Kitendo cha Alfred kumsalimia Shija kwa bashasha, kimechukuliwa kama sehemu ya kampeni, hivyo amerejeshwa jijini Dar es Salaam.

Shija na Alfred, wanafahmiana kutokana na kuwa wanatokea katika taalum moja ya uandishi wa habari.


Hata hivyo, hakuna sehemu inayoonyesha kumsalimia mtu kwa bashasha ni sehemu ya kampeni, huenda ni jambo lililomfanya Alfred kuona hakutakuwa na tatizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV