August 3, 2017


Kikosi hicho chini ya kocha wake mkuu, Joseph Omog,  kinatarajiwa kurejea nchini Agosti 5, mwaka huu kikitokea Afrika Kusini pamoja na Niyonzima ambaye rasmi ametangazwa kuwa atavaa uzi wa timu hiyo akitokea Yanga.

Niyonzima baada ya kujiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili, alienda kwao Rwanda kwa shughuli zake binafsi, na anatarajiwa kuungana na timu yake hiyo mpya mara tu watakapotoka Afrika Kusini.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba, Haji Manara, amezungumza na SALEHJEMBE na kufafanua kuwa kuna uwezekano mkubwa Niyonzima asiende Afrika Kusini.
“Niyonzima anaweza kuungana na kikosi wakati kinarejea kutoka Afrika Kusini maana kitapitia Kigali, Rwanda. 

“Hivi sasa Niyonzima yupo kwao Rwanda na anaendelea kujifua na timu ya APR akisubiri wenzake wampitie Agosti 5, mwaka huu kuja Bongo kujiandaa na Tamasha la Simba Day ambalo litafanyika Agosti 8, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, siku ambayo tutacheza mechi ya kirafiki na Rayon Sport,” alisema Manara.


Manara aliongeza kuwa, kutokana na Niyonzima kuwa bize akishughulikia masuala yake ya kifamilia, kama akimaliza mapema anaweza kwenda Sauz, lakini ikishindikana atasubiri wenzake wampitie kwani ndege ambayo watapanda kuja nayo Tanzania kutoka Afrika Kusini ni Rwanda Air itakayopitia nchini Rwanda

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic