August 19, 2017




 Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Yusuf Manji, jana Ijumaa alishindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili kwa kile kilichoelezwa kutokuwa vizuri kiafya.

Huku Manji akishindwa kufika mahakamani hapo, watuhumiwa wenzake watatu ambao ni Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere, walifika lakini Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa, aliahirisha kesi hiyo mpaka Agosti 25, mwaka huu.

Wakili wa serikali, Estazia Wilson, aliieleza mahakama mbele ya Hakimu Mwambapa kuwa, amepata taarifa kutoka kwa askari magereza kwamba Manji ameshindwa kufika kutokana na kuumwa.

Ikumbukwe kuwa, Manji na watuhumiwa wenzake watatu, wanakabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi cha Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe pamoja na ‘plate number’ mbili za magari ya serikali.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic