August 26, 2017



Na Saleh Ally
UKIANGALIA utaona sasa lile joto la Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’ linaanza kupanda vizuri wakati timu zinaingia kucheza mechi zao za pili za ligi.

Kama ilivyo kawaida, mechi zote za Bundesliga huonyeshwa moja kwa moja kupitia king’amuzi cha Startimes, hali inayofanya wapenda soka wengi nchini waendelee kupata burudani ya ligi hiyo bora zaidi kwa takwimu za uwanjani.

Karibu kila timu itakayocheza, unaweza kusema ina deni. Wale walioshinda wangependa kuendeleza ushindi lakini waliopata sare safari hii watataka kubeba pointi tatu huku wale waliopoteza wakiwa wamelenga kuhakikisha hawarudii makosa tena.

Kuna baadhi ya mechi utaona kuna ugumu zaidi kulingana na mambo yalivyo, huenda timu ilipoteza na inakutana na timu iliyopoteza au timu ilipoteza sasa inakutana na timu ambayo inajulikana kupoteza kwao wanaona ni mwiko.

Bayer Vs Hoffenheim:
Katika mechi za ufunguzi wa msimu wiki iliyopita, Hoffeinheim ilipata ushindi dhidi ya Werder Bremen ambao walikuwa ugenini. Hoffeinheim walionekana kuwa na presha kubwa na mechi ya play-off ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool, wakaweka nje mastaa wao ambao waliwaingiza baadaye na wakasaidia kupatikana kwa ushindi wa bao 1-0.

Waliposafiri kwenda Anfield, Liverpool wakakutana na kipigo cha mabao 4-2 na kutolewa sasa wamerudisha nguvu Ujerumani lakini wanakutana na Bayer ikiwa nyumbani na kumbuka mechi ya kwanza walipigwa 3-1 na wapinzani wao Bayern Munich.

Timu hii inayomilikiwa na watengeneza dawa, Kampuni ya Bayer hawatataka kupoteza tena wakiwa nyumbani na itakuwa ni kazi kwelikweli.

Werder Vs Bayern:
Kama unakumbuka, mechi ya kwanza wakiwa ugenini walipigwa bao 1-0 na Hoffeinhem na baada ya mechi, wachezaji walionekana kusikitika sana kama wamepoteza fainali. Sasa wamerudi nyumbani katika Mji wa Bremen ambao uko Kaskazini ya Ujerumani na inakuwa mechi ya kwanza ya msimu wanacheza nyumbani, lazima washinde.

Bayern wao watataka kuendeleza moto bila ya kujali wako wapi. Hii itakuwa moja ya bonge la game ambalo unatakiwa kutolikosa.

Dortmund Vs Hertha Berlin:
Baada ya ushindi wa 3-0 wakiwa ugenini dhidi ya Wolfsburg, Borussia Dortmund wamerejea nyumbani na wanakutana na Hertha Berlin walioonja ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya VfB Stuttgart.

Hertha wanakuwa ugenini lakini wanajua utamu wa ushindi ni nini. Dortmund wamerejea nyumbani kwenye uwanja unaoingiza mashabiki wengi zaidi kwa karibu kila msimu nchini humo lakini pia barani Ulaya.

Dortmund hawatataka utani lakini Hertha watataka kuendeleza ushindi kwa kuwa wamejenga kujiamini maana wanajua wanaweza kufunga na kulinda wasifungwe kama walivyofanya katika mechi ya kwanza.

Mechi ya RB Leipzig nayo inaonyesha itakuwa ngumu wakiivaa SC Freiburg, timu kutoka Kusini mwa nchini ya Ujerumani. Hii inatokana na kwamba, timu zote mbili hakuna iliyoonja ushindi baada ya Leipzig kupigwa na Schalke 04 na Freibug wakiwa nyumbani wakaambulia sare.

Augsburg walipigwa mechi ya kwanza dhidi ya Hamburger sasa wako nyumbani wakiwavaa Monchengladbach, wabishi hawa katika mechi ya kwanza wakiwa nyumbani walishinda kwa bao 1-0 dhidi ya FC Kolon au FC Kölninayotokea katikati ya Ujerumani.

Ligi hiyo itaanza kuonyesha mwelekeo kupitia mechi za leo kwa kuwa kila timu itataka kujirekebisha na kujiweka sawa. Kwa wale watakaopoteza mechi za pili, watakuwa wamejichimbia ‘kaburi’ kwa kuwa watakuwa wana ugumu baadaye.


Ratiba ya wikiendi hii
         
Agosti 26, 2017
Leverkusen         v       Hoffenheim                  BayArena 10:30 Jioni        
W.Bremen           v       Bayern München         Weser        10:30 Jioni        
Augsburg            v       B. M'gladbach              WWK       10:30 Jioni        
Stuttgart              v       Mainz 05                      Mercedes  10:30 Jioni        
E.Frankfurt         v       Wolfsburg                    Commerz  10:30 Jioni        
B.Dortmund       v       Hertha BSC                  Signal       1:30 Usiku         

Sunday 27 August 2017
RB Leipzig                   v       Freiburg                        Red Bull    10:30 Jioni        
Hannover            v       Schalke 04                    HDI-Arena          1:00 Usiku         


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic