August 17, 2017





Mshambulizi mpya wa Simba aria wa Ghana, Nicholas Gyan amesema yuko tayari kubadili uraia na kuwa Mtanzania.

Gyan ambaye amejiunga na Simba akitokea katika klabu ya Ligi Kuu Ghana ya Ebusua Dwarfs, amesema anatamani kuichezea timu ya taifa na ndoto yake imekuwa ni kucheza timu ya taifa ya Ghana, Black Stars bila ya mafanikio.

Gyan ameuambia mtandao mmoja wa Ghana kwamba kama atapewa nafasi ya kubadili uraia aicheze Tanzania ‘Taifa Stars, yuko tayari kufanya hivyo.

“Kama nilifunga mabao 11, hata nafasi ya kuingia timu ya taifa inakuwa ngumu. Kweli sitaona shida kuhamia kule kwa watakaonipa nafasi,” alisema.

Kabla ya kuja nchini, Gyan aliyefunga mabao 11 katika ligi ya Ghana alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ghana iliyokuwa inajiandaa na mechi ya kuwania kucheza Chan dhidi ya Burkina Faso.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic