Kiungo Mbrazil, Paulinho ameamua kuondoka China na kutua Barcelona kwa day la pauni million 36.5.
Paulinho alikuwa akikipiga Guangzhou Evergrande inayoshiriki China Super League.
Tayari amekabidhiwa jezi namba 15 Camp Nou na Barcelona inaonekana imepania kuongeza nguvu katika kikosi chake kinachoonekana kutokuwa vizuri kama wanavyotaka kabla ya kuanza La Liga.
Pamoja na kukabidhiwa jezi, Paulinho alikabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Audi A7. Kampuni ya Audi ni wadhamini wa Barcelona.
0 COMMENTS:
Post a Comment