August 3, 2017

MAHARAGE CHANDE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI HII LEO.

Multichoice Tanzania kupitia king’amuzi cha DSTv imezindua rasmi Msimu mpya wa Soka” wakitumia kampeni mpya ya “Full Vyenga Bila Chenga”.


Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande aliongoza zoezi hilo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye ofisi zao jijini Dar es Salaam.

Wakati wa uzinduzi alisema wakati wa msimu huo watapunguza bei ikiwa ni pamoja na kuuza king’amuzi cha Sh 79,000 na kinakuwa king’amuzi nafuu zaidi chenye burudani ya uhakika ya soka.

"Maana ya Tazama Vyenga bila Chenga, maana yake kupitia king'amuzi cha DSTv unaona kwa ubora wa juu. Maana yake utaona kila tukio na kama ni vyenga basi unaona bila ya kuwa na chenga.

“King’amuzi hicho pia kitaonyesha matangazo yanayorushwa katika lugha ya Kiswahili ili kuwapa watu nafasi ya kuelewa zaidi,” alisema.

Pamoja na uzinduzi wa kampeni hizo, walieleza namna ambavyo wamekuwa na mafanikio ikiwa ni pamoja na kusaidia Watanzania wengi kuburudika na soka katika ligi mbalimbali kama Premier League ya England, La Liga ya Hispania, Serie A ya Italia, League 1 ya Ufaransa na ligi nyingine mbalimbali.


Chande alisema wamenuia hasa kuendelea kutoa burudani kwa wapenda soka nchini.

Wametangaza kuanza kwa msimu mpya kwa kuwa kuanzia wiki hii, ligi zitaanza na utambulisho wa michuano ya hisani.
MKUU WA MASOKO MULTICHOICE TANZANIA, ALPHA.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV