August 3, 2017


Ungeweza kusema labda Alvaro Morata wa Chelsea ametua Tanzania kwa matembezi wakati Multichoice Tanzania kupitia king’amuzi cha DSTv wakizindua rasmi “Msimu mpya wa Soka” wakitumia kampeni mpya ya “Full Vyenga, Bila Chenga”.

Maana Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande aliyekuwa amevaa jezi ya Chelsea, mabingwa wa England ambao sasa wanamtegemea Morata katika ushambulizi, alivyoonyesha yake.

Chande ambaye licha ya kuwa bosi lakini ni mwanamichezo, alipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake wa kumiliki mpira mbele ya wafanyakazi wenzake na wanahabari, naye akasema yuko tayari.

Baada ya hapo akakabidhiwa mpira, naye akafanya yake utafikiri Morata alipowasili Chelsea siku ya utambulisho baada ya kusajili.

Waandishi na wafanyakazi wa Multichoice Tanzania walijikuta wakipiga kelele kumshangilia wakati akijaribu kuonyesha manjonjo ya kuumiliki mpira kutumia viungo vyake mbalimbali.


1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV