August 24, 2017



Aliyekuwa mgombea wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Shija Richard amewataka waliopata nafasi ya kuliongoza, wahakikishe kuna mipango ya muda mfupi na mrefu badala ya kutaka kushika kila kitu.

Shija amesema, kama TFF watataka kufanya kila kitu ndani ya miaka minne pekee, hawataweza.

“Miaka minne ni michache sana, hauwezi kufanya kila kitu. Badala yake kutakuwa na mambo ambayo wanatakiwa kufanya.

“Inawezekana wataendelea wao au uongozi mwingine ukaingia na kuendeleza. Wakitaka wafanye kila kitu ndani ya miaka minne, mwisho watamaliza kila kitu kikiwa hakijafanyika,” alisema.

Shija alishindwa katika uchaguzi Mkuu wa Viongozi TFF ambao ulifanyika mjini Dodoma Agosti 12 na Wallace Karia akashinda kuwa rais huku Michael Wambura akitwaa nafasi ya makamu wa rais.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic