August 6, 2017Licha ya kuwa jijini Dar es Salaam, Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima, hawajatokea katika mazoezi ya Simba leo.
Simba imefanya mazoezi yake ya kwanza jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tokeo irejee ikitokea nchini Afrika Kusini ilikoweka kambi.
Simba imefanya mazoezi kwenye Viwanja vya Gymkhana kukiwa na ulinzi na wanahabari wakizuiwa kuingia.
Taarifa zinaeleza, Okwi na Niyonzima wamefichwa, huenda wakaanza mazoezi kesho kwa kufanya mazoezi mepesi kabla ya Simba Day keshokutwa.
Taarifa zinaeleza, katika mazoezi hayo Simba watazuia vyombo vya habari kuingia ili kuhakikisha wachezaji hao wanaanza kuonekana Jumanne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV