August 6, 2017


Pamoja na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United katika mechi yao ya kwanza ya kirafiki jijini Dar katika kipindi cha maandalizi, kocha wao, bado anataka kubadilisha mambo.
Kocha George Lwandamina amepanga kuhakikisha Yanga inapata mabao ya haraka badala ya kwenda na mwendo wa kusawazisha kama ambavyo Yanga ilifanya.
Yanga ililazimika kusawazisha kupata matokeo ya 2-2 kabla ya kufunga bao katika dakika za mwisho na kuibuka na ushindi.
“Kocha anataka mabao ya haraka, amesisitiza suala la kutangulia kufunga ili kuumiliki mpira,” kilieleza chanzo tokea ndani ya Yanga.

“Kuanzia Jumatatu tutajipanga na masuala ya ulinzi na kufunga mabao mapema. Kocha amesema kuruhusu kufunga mapema ni kuwapa nafasi wengine kutawala mchezo kwa maana ya kujipa presha.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV