August 1, 2017Vyombo via habari barani Ulaya vimeendelea kuweka msisitizo kwamba mshambulizi wa Barcelona, Neymar, lazima atajiunga na PSG ya Ufaransa.

Kuonyesha msisitizo wa hilo, vingi vimetengeneza picha zikionyesha namna Neymar anavyofurahia kujiunga na timu hiyo ya Ufaransa.

Taarifa za mwanza zimeelezwa ndani ya saa 48 kwa asilimia 80 inaonekana Neymar atakuwa mchezaji wa PSG ya Ufaransa.

Taarifa zinaeleza, Barcelona iko katika nafasi ya kumuachia Neymar ili kuepuka kumlipa baba mzazi wa mchezaji huyo, Neymar Sernior kitita cha pauni milioni 26.


Katika mkataba alioingia na Barcelona akitokea Santos ya kwao Brazil, unaeleza kuwa kama akiongeza mkataba mpya na Barcelona, basi baba yake huyo ambaye ni meneja wake anapaswa kulipa kitita cha pauni milioni 26.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV