September 13, 2017



Benchi la ufundi la Majimaji limewapa maagizo maalum mabeki wa timu hiyo chini ya kitasa wao, Tumba Sued kuhakikisha kuwa wanatumia mbinu zao ili kuizima safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo inaongozwa na Donald Ngoma na Ibrahim Ajibu, wasipate bao kwenye mchezo wao wa wikiendi hii.

Majimaji ambao wanafundishwa na kocha Habibu Kondo watakuwa wenyeji wa Yanga wikiendi hii kwenye mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa Uwanja wa Majimaji, Songea mkoani Ruvuma. Mara ya mwisho vikosi hivi vilipokutana uwanjani hapo Yanga walishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Deus Kaseke.

Chanzo kutoka ndani ya timu hiyo kimesema kuwa wameiona safu ya ushambuliaji ya Yanga kwenye mchezo wa Njombe Mji, hivyo na kuona safu hiyo ya ushambuliaji ndiyo inaibeba timu hiyo ndiyo maana wameweka mikakati maalumu ya kuhakikisha hawafurukuti mbele yao.

“Yanga tumewaona tulivyokuwa hapa Njombe kwenye mchezo wao na Njombe Mji na tumebaini kuwa uzuri wao na uhai wa timu upo kwenye maeneo mawili eneo la kiungo ambapo msumbufu ni yule Thaban Kamusoko na ushambuliaji ambapo yupo Ajibu.


“Sasa baada ya kuyabaini hayo tumeandaa mkakati mzito kuhakikisha kuwa tutakapocheza nao wikiendi hii basi hawaleti madhara na tayari walinzi wetu wameonyesha dalili kubwa ya kuelewa kile ambacho tunawapa ili tu wapinzani wetu hao wasiweze kutufunga,”kilisema chanzo hicho.  

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic