September 13, 2017


Bosi wa benchi la ufundi la Azam FC,  Mromania, Aristica Cioba amefunguka kuwa matokeo ya sare dhidi ya Simba yamempa mwanga na kuona ubora wa kikosi chake.

Azam imetoka sare ya bila kufungana na Simba katika mchezo uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar ambapo wamefikisha pointi nne sawa na Simba na Yanga ambao wote wamecheza mechi mbili.

Cioaba alisema kuwa matokeo yao yamempa mwanga na ukubwa wa kikosi chake tofauti na msimu uliopita hali ambayo naamini wanaweza kufanya makubwa msimu huu.

“Matokeo ya sare dhidi ya Simba kwetu ni bora kwa sababu kwanza yamenifanya nijue ubora wa kikosi changu ambacho ni tofauti na kile cha msimu uliopita ambacho hatukuweza kufanya vizuri maana Simba siyo timu ya kubeza kutokana na  aina ya wachezaji wake.


“Ubora wa matokeo yetu unatokana na mchezo ulivyokuwa kwa sababu wao waliweza kutawala mchezo kipindi cha kwanza lakini  kipindi cha pili chote tulitawala sisi baada ya kuongea na wachezaji wangu, nadhani kwa matokeo haya kwetu ni faida kubwa yakuweza kufanya vizuri msimu huu,” alisema Cioaba

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic