September 13, 2017



Dereva wa basi la Simba, Nassor maarufu kama Chollo ni mgonjwa na amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa zinaeleza, Chollo anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na hali ya si nzuri sana.

Lakini Meneja wa Simba, Cosmas Kapinga amesema ni suala la kusubiri vipimo.

"Ni kweli amelazwa kwenye taasisi ya moyo. Lakini mimi ni daktari siwezi kukubali tu kuwa ni tatizo la moyo.

"Nikipata vipimo ndiyo naweza kulizungumzia, hivyo sasa ni vizuri kama tutasubiri vipimo ili niseme kipi kinachomsumbua," alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic