FULL TIME
Mchezo umemalizika, Yangaa imepata ushindi wa bao 1-0.
Mwamuzi anamaliza mchezo.
Dakika ya 91: Baadhi ya mashabiki wameanza kutoka nje ya uwanja.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 89: Yondani anacheza faulo karibu na lango lake, mwamuzi anaamuru ipigwe faulo, inapigwa inatoka nje.
Dakika ya 85: Chirwa anapata nafasi lakini walinzi wa Njombe wanamuwahi.
Dakika ya 80: Mchezo ni mkali na umebalansi kwa timu zote kupokezana kushambuliana.
Dakika ya 77: Njombe wanaonyesha uhai na kutengeneza mashambulizi lakini wanakosa umakini katika kumalizia.
Dakika ya 70: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Emmanuel Martine, anaingia Yusuph Mhilu.
Dakika ya 56: Obrey Chirwa anaingia, anatoka Donald Ngoma.
Dakika ya 54: Mchezo umesimama kwa muda, kuna mchezaji wa Njombe yupo chini anatibiwa, aliumia alipokuwa akiwania mpira na Mahadhi.
Dakika ya 53: Njombe wamerejea wakiwa na nguvu kubwa, wamefanya mashambulizi mawili ndani ya muda mfupi.
Dakika ya 49: Rafael Daud ameingia kuchukua nafasi ya Kamusoko.
Kamusoko anashindwa kuendelea, anatoka, anakabidhi kitambaa cha unahodha kwa Yondani.
Dakika ya 48: Thaban Kamusoko wa Yanga yupo chini, anaonyesha ameumia.
Dakikaya 46: Kiungo wa Yanga, Tshishimbi anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo.
Mchezo umeanza, kipindi cha pili.
Wachezaji wanarejea uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili.
MAPUMZIKO
Dakika ya 47: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.
Dakika ya 46: Njombe wanafanya shambulizi kali, shuti kali linapanguliwa na kipa wa Yanga, kisha walinzi wa Yanga wanaokoa.
Dakika ya 45: Zinaongezwa dakika mbili za nyongeza.
Dakika ya 45: Njombe wanashindwa kutengeneza nafasi za kufunga.
Dakika 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.
Dakika ya 39: Njombe wanapata nafasi lakini shuti linatoka nje ya lango.
Dakika ya 34: Walinzi wa Njombe wanaonyesha kujiandaa kumdhibiti Ngoma, muda wote wapo naye.
Dakika ya 27: Mchezo una kasi kiasi, Juma Mahadhi na Emmanuel Martin wanabadilishana winga.
Dakika ya 24: Gadiel Michael wa Yanga ameingia na mpira lakini beki wa Njombe anamuwahi na kuutoa mpira.
Mashabiki wa Yanga wameamka kwenye siti zao wakishangilia kwa nguvu.
Ibrahim Ajibu anaipatia Yanga bao la kwanza kwa kupiga faulo ambao imeenda wavuni moja kwa moja.
Dakika ya 16: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dakika ya 15: Yanga wanafika langoni mwa Njombe mara kadhaa.
Dakika ya 10: Matokeo bado ni 0-0 mchezo una kasi ya kawaida.
Dakika ya 5: Bado timu zote zinasomana taratibu.
Mchezo umeanza/
Timu zinaingia uwanjani.
Huu ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Njombe Mji ipo nyumbanji ikiikaribisha Yanga.
Hujatulia hata kidogo. Siku hizi huwezi tena kutuletea uhondo kamili.
ReplyDelete