September 10, 2017





Na Saleh Ally, London
Mashabiki wa Arsenal wamewazomea kwa nguvu mashabiki wenzao wa Arsenal baada ya timu yao kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Bournemouth kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, jana.

SALEHJEMBE blog iliyokuwa uwanjani hapo, ilishuhudia mashabiki wengi wa Arsenal wakiwazomea wale ambao wamekuwa wakisisitiza Kocha Arsene Wenger aondoke.

Mara baada ya Arsenal kupata bao la pili, mashabiki hao walianza kupiga kelele wakiwazomea mashabiki hao na walipafanya hivyo baada ya kupata bao la tatu.

Kama haitoshi, walizidi kuwazomea baada ya mechi kwisha na mashabiki hao walioingia uwanjani na mabao yao walionekana kuyakunja huku wakiwa kimya.

Imeelezwa mashabiki hao huwa na sehemu maalum na kampeni yao ni kuhakikisha Wenger anafutwa kazi.


Arsenal ilionyesha soka safi katika mechi hiyo na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo safi mabao mawili yakifungwa na Danny Welbeck na moja Alexandre Lacazette.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic