September 5, 2017




Mashabiki wa soka wamelalamika kitendo cha mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Azam FC kupelekwa Azam Complex, Chamazi.

TFF imeamua kutangaza michezo ya Simba na Yanga dhidi ya Azam FC, sasa nayo itakuwa inachezwa Azam Complex tofauti na awali kutokana na ukubwa wake ilitakiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa au ule wa Uhuru. 

Safari hii, Azam FC itaikaribisha Simba Chamazi katika mechi itakayopigwa Jumamosi ikiwa ni ya pili ya Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kila timu.

Mashabiki hao walioandika maoni katika mitandao ya Kijamii ya Salehjembe pamoja na blog yenye ya Salehjembe wamelia kutotendewa haki.

Kwa ujumla mashabiki hao wamelalamika kuhusiana na udogo wa uwanja wa Azam Complex wenye uwezo wa kuchukua watu 7,000.

“Nafikiri hii si sawa, wote tunajua uwanja huo ni mdogo na hii ni mechi kubwa. Wanatunyima haki ya kuona mechi hiyo.

“Angalau kungekuwa hakuna viwanja, lakini kuna Uhuru upo pale.”

Wengine walilalamikia umbali wa Chamazi na muda ambao mechi imepangwa Saa 1 usiku.

Lakini Azam FC imekuwa na kilio cha kutaka kucheza mechi zake nyumbani jambo ambalo hatimaye limetimia.




4 COMMENTS:

  1. Hakuna kitu kinachotakiwa kama usalama wa watu,nilikuwa shuhuda wkt ajali ikitokea kule south africa kutikana na uwanja kuzidiwa na umati mkubwa wa mashabiki, Azam complex ni ueanja mdogo mno na mechi ni kubwa, mbaaya sana eti askari watakuwepo pale kuhakikisha uwanja usijae, isitoshe muda wa kuanza mchezo saa moja jioni, nawaasa TFF wasiangalie kilio cha upande mmoja kuleta maafa, mpira wa miguu una wapenzi wengi sana kuliko mchezo mwingine

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umetoa ushauro mzuri sana kama watausoma, otherwise tusubirie kamati za uchunguzi baada ya maafa, alieturoga kafa sie

      Delete
    2. Yanga/Simba acheni kulialia Jengeni viwanja vyenu. sio mnategemea viwanja vya serikali ambavyo kukiwa na Mahubiri, sherehe za Chama au wenyewe wakikasirika tu Hakuna Kucheza. Nendeni chamazi Mkajifunze.. Suala la Usalama ni la Serikali

      Delete
  2. Kingine ni kuwa mtu anaweza kufunga safari mpaka chamazi saa 1 usiku, akafika kule akaambiwa uwanja umejaa. Ni rahisi kusema Simba na Yanga zinapendelewa lakini lazima tuwe wakweli kuwa miundombinu yetu bado haijawa sawa kuruhusu kila timu kucheza kwenye uwanja wake. Ila lazima pia tuheshimu kuwa Azam wana haki ya kuchagua uwanja. Bado sidhani kama ilikuwa busara sana kushikilia msimamo huo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic