September 4, 2017


KWA sasa wengi wanamuona Gary Neville akikosoa na kusifia katika uchambuzi wake wa soka kwenye vituo vya televisheni, lakini waliomuona gwiji huyu akicheza, ndio wana stori nzuri zaidi ya kusimulia.  Gary Alexander Neville, aliyezaliwa Februari 18, 1975, ni nyota wa zamani Muingereza, aliyecheza soka katika klabu moja tu ya Manchester United lakini kwa mafanikio makubwa. 

Hadi anastaafu soka mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 36, Neville alikuwa mchezaji wa pili kwa kuitumikia Manchester United kwa muda mrefu zaidi nyuma ya Ryan Giggs, na alitumika kama nahodha wa klabu hiyo kwa miaka mitano. Heshima ya Neville, 42, ni kubwa mno katika kikosi cha Manchester United pamoja na timu ya taifa ya England. 

Akichukuliwa kama mmoja wa magwiji wanaoheshimika Old Trafford, Neville alishinda jumla ya mataji 20 katika maisha yake ya soka, yakiwemo nane ya Ligi Kuu England (Premier) na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 Kuhusu timu ya taifa, Neville alianza kuichezea England mwaka 1995 na alikuwa beki wa kulia
chaguo la kwanza kwa zaidi ya miaka 10 kabla ya kustaafu kwake mwaka 2007. Aliliwakilisha taifa hilo kwenye michuano mitatu ya Ulaya (Euro) mwaka 1996, 2000 na 2004, kote huko akiwa chaguo la kwanza, pia alicheza kwenye Kombe la Dunia 1998 na 2006 (ingawa katika Kombe la Dunia 2006 alicheza mechi mbili tu –moja ya hatua ya makundi na moja ya robo fainali - kutokana na majeraha). 


Licha ya kuikosa michuano ya Kombe la Dunia 2002 kutokana na majeraha, Neville ni beki wa kushoto aliyeichezea E n g l a n d mechi nyingi zaidi kihistoria akiwa amecheza jumla ya mechi 85. Katika kikosi cha Manchester United ambako ndiko alikotengeneza jina, Neville alijiunga na timu hiyo katika kikosi cha vijana akitokea shule mwaka 1991, lakini alipambana na kufanikiwa kuwa beki wa kulia chaguo la kwanza kuanzia msimu wa 1994-1995 chini ya kocha Sir Alex Ferguson. 

Neville alikuwa mmoja wa makinda walioibuliwa na Ferguson kwenye miaka ya 1990, akiwa na ndugu yake Phil Neville, Ryan Giggs, David Beckham, Nicky Butt na Paul Scholes, walijulikana kama ‘Class of 92’.

 Akimzungumzia Neville, kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, anasema: “Gary alikuwa beki wa kulia Muingereza bora zaidi katika kizazi chake.” Neville alikuwa akielewana vizuri na Beckham wakicheza pembeni wakati huo winga huyo
alipokuwa akicheza namba saba. Neville alikuwa akipanda na kumpa asisti nyingi. Neville alikuwa nahodha wa United kuanzia 2005 baada ya kutimka kwa Roy Keane aliyezinguana na Ferguson. Aliifanya kazi hiyo hadi 2010. 


Mwaka 2007, gwiji huyo alianza kusumbuliwa na majeraha. Baada ya kukaa nje kwa muda mrefu, Aprili 9, 2008, Neville alirejea dimbani katika mchezo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma. Alipoingia dakika ya 81 kuchukua nafasi ya Anderson, mashabiki walisimama na kumpigia makofi. Hiyo ilikuwa ni mechi ya 99 ya Uefa kwa bro huyo. Hata hivyo, hakuteuliwa katika fainali Mei 21 dhidi ya Chelsea, lakini alijumuika kushangilia ushindi wa penalti, baada ya sare ya 1-1 hadi muda wa nyongeza. Rio Ferdinand na Giggs ndiyo walioanza kulinyanyua kombe hilo kwa pamoja, kwa kuwa walibadilishana unahodha wakati wote ambao Neville hakuwepo.

 Kutokana na kushindwa kucheza mara kwa mara kwa sababu ya majeraha, Neville alikivua kitambaa cha unahodha mwaka 2010 akimpa ama Rio Ferdinand, Nemanja Vidić au Patrice Evra, hata hivyo alibaki kuwa nahodha nje ya uwanja. Neville aliamua kustaafu mapema akiwa na miaka 36, kutokana na majeraha ya mara kwa mara. MATAJI Manchester United Premier League (8): 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07,
10

MAISHA HALISI...
BEKI NOMA ALIYEBEBA MATAJI 20 MAN U 2008–09 FA Cup (3): 1995–96, 1998– 99, 2003–04 Kombe la Ligi (2): 2005–06, 2009–10 Ngao ya Jamii (3): 1996, 1997, 2008 Ligi ya Mabingwa Ulaya (2): 1998–99, 2007–08 Intercontinental Cup (1): 1999 Kombe la Dunia la Klabu (1): 2008 MAISHA BINAFSI Baba yake Neville, marehemu Neville Neville, alikuwa mchezaji wa kulipwa wa kriketi, wakati mama yake, Jill, alikuwa akicheza netiboli katika ligi za ndani, pia ni meneja mkuu na katibu wa timu ya Bury. Dada yake, Tracey Neville, alikuwa akicheza netiboli kimataifa. Neville alikuwa mtaalamu wa kucheza kriketi alipokuwa shule. Neville amemuoa mrembo Emma Hadfield, na wana watoto wawili wa kike (Molly, aliyezaliwa Jan 11, 2009 na Sophie, aliyezaliwa Machi 25, 2010). Julai 2009, Neville alitunukiwa digrii kutoka Chuo Kikuu cha Bolton kutokana na mchango wake katika soka. ANACHOKIFANYA KWA SASA Neville ni mmiliki mwenza wa Klabu ya Salford City akiwa pamoja na magwiji wenzake Ryan Giggs, Paul Scholes, Nicky Butt na Phil Neville. Neville pia amewahi kuwa kocha msaidizi wa England na kocha mkuu wa Valencia. Lakini kazi kubwa anayoifanya kwa sasa ni uchambuzi wa 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic