September 4, 2017



MIONGONI mwa wachezaji waliofanikiwa kuandika rekodi za pekee katika mechi za kwanza za Ligi Kuu Bara msimu huu, ni mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi. 


Okwi ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea SC Villa ya Uganda kwa dau la Sh milioni 115, alifanikiwa kuandika rekodi ya kufunga zaidi ya mabao matatu ‘hat trick’ katika ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting na kuibuka na ushindi wa mabao 7-0. Okwi pekee alifunga mabao manne.


 Ndiye mchezaji pekee aliyefunga hat trick hadi sasa msimu huu. Hata hivyo, licha ya kufanya hivyo, Okwi bado ana mtihani mkubwa wa kufanya ili aweze kumfikia mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe. Kama ulikuwa hujui, Tambwe ndiye bingwa wa kufunga hat trick kwa wachezaji wa sasa wanaoshiriki ligi kuu. 
Tambwe ndiye anayeshikilia rekodi ya kufunga hat trick mara mbili ndani ya msimu mmoja wa ligi kuu na amefanya hivyo katika misimu mitatu mfululizo, tangu alipotua hapa nchini msimu wa 2013/14. 


Katika msimu wake wa 2013/14, Tambwe alifunga hat trick mbili, ya kwanza ilikuwa dhidi ya Mgambo JKT ya Tanga ambapo Simba ilishinda mabao 6-0 huku yeye akifunga mabao manne, ya pili ilikuwa dhidi ya JKT Oljoro, katika mechi hiyo Simba ilishinda 4-0  na yeye alifunga mabao matatu.

 Msimu wa 2014/15 akiwa Yanga, hat trick ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Coastal Union ambapo Yanga ilishinda mabao 8-0 huku yeye akifunga mabao matano, hat trick ya pili msimu

kwa kazi yake hiyo nzuri aliyoifanya katika kipindi hicho. “Binafsi natamani sana na mimi nifanye kama yeye msimu huu na ikiwezekana nivunje kabisa rekodi hiyo ya kufunga hat trick mbili ndani ya msimu mmoja. 

“Naamini uwezo wa kufanya hivyo ninao ila kikubwa ni uzima, japokuwa najua haitakuwa kazi nyepesi lakini uwezo ninao mkubwa,” a n a s e m a Okwi. B a a d a ya maneno
hayo ya O k w i , Tambwe n a y e anasem a : “ N a m shukuru s a n a O k w i k w a pongezi z a k e hizo na ninamtakia jitihada njema katika kutimiza lengo lake hilo lakini pia binafsi natamani pia kuiendeleza rekodi hiyo msimu huu baada ya msimu uliopita kushindwa kufanya hivyo.

 “Namuomba Mungu anijalie afya nje ili msimu huu nisipate majeraha ya mara kwa mara kama ilivyokuwa msimu uliopita lakini nipate nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza.” Kwa upande wake Mussa ambaye ni mfungaji bora msimu uliopita, anasema: “Nimejipanga vizuri na ni matumaini yangu nitafunga tena hat trick msimu huu licha ya Okwi kuwa tayari ameshafanya hivyo lakini na mimi nataka nifanye hivyo.

” Mussa, katika mechi ya kwanza ya ligi kuu msimu huu, hakuweza kuitumikia timu yake ya Ruvu Shooting dhidi ya Simba ilipofungwa mabao 7-0. Kwa upande wake Kiduku anasema: “Natamani sana kufanya hivyo lakini kwa jinsi hali ya ushindani ilivyo hakika nina mtihani mkubwa lakini nitapambana vilivyo ili niweze kuandika rekodi hiyo kwa mara nyingine tena msimu huu.”
Dar es Salaam huo ilikuwa dhidi ya Polisi Moro ambapo Yanga ilishinda kwa mabao 4-1, mabao matatu kati ya hayo aliyafunga yeye pia. Msimu wa 2015/16 alifanya hivyo tena baada ya kuiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United ambapo yeye alifunga mabao matatu na hat trick yake ya pili msimu huo ilikuwa dhidi ya Majimaji  ya Songea kwenye Uwanja wa Taifa katika ushindi wa mabao 5-0 huku yeye akifunga mabao matatu. 

Hata hivyo, msimu uliopita haukuwa mzuri kwake kwani hakuweza kufunga hat trick yoyote na kuwaachia Kelvin Sabato ‘Kiduku’ ambaye sasa anaitumikia Mtibwa Sugar pamoja na AbdulrahmanMussa wa Ruvu Shooting. Kiduku alifunga hat trick hiyo wakati alipokuwa akiitumikia Stand United ya Shinyanga katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ilipopambana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro na k u i w e z e sha timu yake hiyo kutoka sare ya mabao 3-3 ikiwa ugenini wakati Mussa yeye alifanya hivyo dhidi ya M a j i maji ya Songea katika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi ambapo aliiwezesha timu yake hiyo ya Ruvu Shooting kuibuka na ushindi wa mabao 4-1. “Nilikuwa sijui kama Tambwe ana rekodi hiyo, hakika anapaswa kujivunia kwa hilo lakini pia nampongeza

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic