September 18, 2017



Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrak Nsajigwa, ameulalamikia Uwanja wa Majimaji kwa kusema una sehemu mbovu ya kuchezea ‘pitch’.

Nsajigwa ambaye ni beki wa zamani wa Yanga, aliyasema hayo baada ya mchezo baina ya timu yake dhidi ya Majimaji kwenye uwanja huo katika kipute cha Ligi Kuu Tanzania Bara, juzi Jumamosi mjini Songea.

Katika mchezo huo Yanga ilipata sare ya bao 1-1 licha ya kuwa yenyewe ndiyo ambayo ilitangulia kufungwa, lakini ilishindwa kucheza soka la pasi muda mwingi kutokana na mara kadhaa mpira kutoelekea katika njia yake kama mpigaji alivyotaka.

“Nashangaa nyie (waandishi) mpo na mnatembelea viwanja vingi tu sijui hamlioni hili linalotokea! Uwanja ni mbovu na mamlaka zimefunga macho juu ya hilo, nafikiri siyo sawa,” alisema Nsajigwa ambaye pia ni nahodha wa zamani wa Taifa Stars.

Kabla ya mpambano huo, uongozi wa uwanja huo ulikuwa bize ukifanya marekebisho ya uwanja huo ikiwemo kumwagilia maji kwa siku mbili mfululizo, kupunguza nyasi kwa mashine maalum na kufanya usafi pembezoni mwa uwanja huo.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic