September 18, 2017



Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amekwenda moja kwa moja hadi katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kuteta na bosi wake wa zamani, Yusuf Manji.


Lwandamina alikutana na Manji katika viwanja vya mahakama ya Kisutu akiwa ameongozana na wasaidizi wake kam Shadrack Nsajigwa akiwemo Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali 'Mensah' na Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh.


Manji alikuwa mahakamani hapo kutokana na Kesi inayomkabiri Manji kuhusiana na kutumia madawa ya kulevya imeshindwa kusikilizwa leo katika mahakama ya Kisutu na kusogezwa mbele hadi Septemba 25.

Suala la kushindwa kusikilizwa ,limetokana na Manji kuchelewa kufika mahakamani, lakini naye alimueleza hakimu kuwa aliambiwa hakimu yuko katika kikao.

Kutokana na hali hiyo, imesogezwa mbele hadi Septemba 25, Manji atakapotakiwa kuleta mashahidi wake.



Manji anatuhumiwa kutumia madawa ya kulevya, jambo ambalo amekuwa akilikanusha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic