September 16, 2017





Bosi wa chama kimoja cha ngumi, juzi alinusurika kuchezea kichapo kutoka kwa bondia Francis Miyeyusho kufuatia kudaiwa kuhusika kuzuia safari yake ya kuelekea Hungary.

Tukio hilo lilitokea juzi baada ya Miyeyusho na bondia mwingine, Saleh Mkwelekwa kuzuiwa na maofisa wa uhamiaji kuingia kwenye ndege muda mchache kabla ya safari yao.

Mabondia hao walizuiwa kusafiri kutokana na kutokuwa na vibali kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambavyo inadaiwa kiongozi huyo ndiye aliyepeleka taarifa hizo.

Bondia huyo ambaye leo Jumamosi alitakiwa kupanda ulingoni kupigana na Zoltan Kovacs, ameliambia Championi Jumamosi kuwa alitaka kumchapa makonde kiongozi kwani ndiye aliyewatibulia.

Alisema kiongozi huyo amemsababishia hasara kwa kuzuia safari hiyo huku akijua wamefuata taratibu zote hapo kabla.

 “Nashindwa kumuelea huyu kiongozi anataka kuniingiza kwenye migogoro yao na vyama vingine ambao hawaelewani navyo, vibali  vyote  tulikata lakini yeye ameamua kudanganya tu.

“Alifika pale uwanja wa ndege (wa Kimataifa wa Julius Nyerere) na kuwaeleza wahusika nasi tukazuiwa kusafiri, ajue siwezi kukubaliana naye na ndiyo maana nilikuwa na hasira za kutaka kumpiga.

“Nimetumia Sh 600,000 kwa maandalizi ya safari, na sijui kwa kuzitoa lakini nakwenda kumfungulia kesi ili anilipe kwa sababu yeye ndiyo tatizo,” alisema Miyeyusho.

Alipotafutwa kiongozi huyo ili kupata ufafanuzi wa suala
hilo ambapo alisema: “Siwezi kukuambia chochote kuhusiana na kilichotokea.”

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic