September 20, 2017



Rashid Mohammed, Mwanza
Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi yake ya mwisho leo kabla ya kuivaa Mbao FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara jijini Mwanza, kesho.

Simba imefanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa kama ambavyo sheria za Fifa zinaangiza timu “mgeni” kufanya mazoezi kwenye uwanja utakaotumika kwa mechi, siku moja kabla.

Kikosi chote cha Simba kimeonekana kuwa fiti na tayari kwa ajili ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu.

Mbao FC wao wamekuwa wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Butimba kujiandaa na mechi hiyo.

Simba tayari wamecheza mechi tatu, wakishinda mbili na sare moja na mechi hiyo dhidi ya Mbao FC itakuwa ya kwanza nje ya Dar es Salaam kwa msimu huu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic