Muda mfupi baada ya Yanga kufanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Njombe Mji FC, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wameamua kuendelea kubaki mkoani Njombe ili kujiandaa kwa mchezo wao ujao.
Yanga ilipata ushindi huo Jumapili hii baada ya Ibrahim Ajibu kufunga bao kwa njia ya faulo katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.
Ofisa Habari wa Yanga, Dismass Ten amesema kuwa wamemaua kubaki mkoani humo ili kujiandaa vizuri kwa mchezo ujao dhidi ya Majimaji ambapo utapigwa kwenye Uwanja wa Majimaji, Ruvuma.
Akifafanua zaidi Dismas alisema: “Tutakuwepo hapa Njombe kwa muda, tunajiandaa kwa mchezo wetu ujao, wachezaji wetu wako fiti na wanaendelea na mazoezi.”

tujipange poa ni muda wa kuzichnga karata waache wapiga domo
ReplyDelete