September 11, 2017





Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa Limited imetoa mchango wa vifaa vya michezo kwa timu ya mpira wa miguu ya Polisi leo tarehe 6 Septemba 2017 katika ofisi zao zilizoko Posta jijini Dar es Salaam.



Akiongea na wanahabari, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania Bwana. Tarimba Abbas amesema,”Tunatambua mchango wa timu ya Polisi Tanzania kwa jamii kiujumla kwani wanafanya kazi kubwa sana kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa bila kuvunjwa.


“Kampuni ya SportPesa itatoa kiasi cha shilingi milioni 20 na jezi kwa timu ya Polisi Tanzania ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali ili kuiimarisha timu hiyo kwani tumedhamiria kuendeleza na kukuza mpira wa miguu nchini kwa kutoa msaada kwa timu mbalimbali.”

Akizungumza kwa niaba ya timu ya mpira wa miguu ya Polisi, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro amesema “Tunapenda kutanguliza shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya SportPesa kwa mchango wao kwenye timu yetu kwani ni kampuni chache sana ambazo zimeweza kutambua mchango wa timu za mpira wa miguu nchini.”

“Tunawaahidi hatutawaangusha kwani timu yetu ilikuwa na uhaba wa vifaa mbalimbali kwa hiyo fedha walizotuchangia zitatumika kuziba mapengo mbalimbali yanayokwamisha timu yetu, hivyo basi kwa niaba ya uongozi wa timu ya Polisi, tunawashukuru sana.”



Sambamba na mchango huo kwa timu ya Polisi, SportPesa ambayo ni kampuni ya michezo ya kubashiri nchini pia inavidhamini vilabu vya Simba, Yanga na Singida United tangu ilipoanza rasmi uendeshaji wa shughuli zake za kibiashara nchini Tanzania, Mei 9 mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic