October 23, 2017



Cristiano Ronaldo amelitetea taji lake la mwanasoka bora wa Fifa safari hii kwa mwaka wa pili mfululizo.

Ronaldo aria wa Ureno na mshambulizi nyota wa Real Madrid amemshinda Lionel Messi aria wa Argentina anayekipiga Barcelona aliyeshika nafasi ya pili.


Nafasi ya tatu imekwenda kwa mwanasoka ghali zaidi duniani, Neymar kutoka Brazil anayekipiga PSG ya Ufaransa.



Ronaldo amefunga mabao 44 kwa klabu na nchi yake. Alifunga mabao mawili katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus na kuiwezesha Real Madrid ya kuweka rekodi ya kubeba Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu miwili mfululizo likiwa ni kombe lao la 12.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic