October 18, 2017




Ili kuhakikisha unatengeneza nidhamu ya timu, uongozi na Benchi la Ufundi la Yanga, hivi karibuni lilimpa onyo kali mshambuliaji wake tegemeo, Ibrahim Ajibu.

Hiyo, ikiwa ni saa chache tangu mshambuliaji huyo apewe kadi ya njano ya makusudi kwa kuvua jezi akiwa anashangilia bao lake la kuongeza dhidi ya Kagera Sugar, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-1.

Ajibu alijiunga na Yanga kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Simba kwa dau la shilingi milioni 50.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani za Yanga zinaeleza, mapema Ajibu alipewa tahadhari kuhusiana na kupata kadi kayika mchezo huo.


 “Viongozi wa benchi la ufundi mara baada ya mechi ya ligi kuu dhidi ya Kagera walikaa kikao kuzungumza na Ajibu na kikubwa alitahadharishwa na hali ya timu kukosekana baadhi ya washambuliaji muhimu kutokana na majeraha ambayo huenda yakawaweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

“Hivyo, basi na hii kadi ya njano aliyopewa Ajibu imewashtua viongozi na kumuita kuzungumza naye na kikubwa walimtahadharisha juu ya kadi za njano zisizokuwa na ulazima ambazo huenda zikatuharibia mipango yetu pale anapokosekana mchezaji muhimu kama yeye katika timu.

“Kama unavyoona Tambwe na Ngoma majeraha yao bado hayajapona vizuri na huenda yakawaweka nje muda mrefu na akaja akapewa kadi ya njano Ajibu utaona ni jinsi gani kikosi chetu kitakavyobomoka katika safu ya ushambuliaji, hivyo basi tayari tumemuonya katika hilo katika 
kutengeneza nidhamu ya timu,” alisema mtoa taarifa huyo.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic