Kiungo Thabani Kamusoko anatarajia kuungana na kikosi cha Yanga leo.
Kamusoko aliyekuwa majeruhi alilazimika kupumzishwa mechi zote mbili za Kanda ya Ziwa dhidi ya Kagera mjini Bukoba na Stand United mjini Shinyanga.
Lakini sasa anaungana na wenzake Morogoro kwa ajili ya kambi kujiandaa na Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara, Jumamosi.
“Kamusoko naye anaungana na wenzake, atakuwa amepona na alikuwa anafanya mazoezi mepesi.
“Sasa anaungana na wenzake ili kufanya maanalizi ya mwisho,” kilieleza chanzo.
Kamusoko ni kiungo muhimu upande wa Yanga hasa katika ukabaji na ugawaji mipira kwa haraka na lazima kumtumia kwa kuwa Yanga inakutana na Simba inayotumia viungo wengi zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment