October 18, 2017



Ikiwa bado siku 10 sawa na sasa 244, timu za Simba na Yanga zikutane kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Bara msimu huu utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo ambayo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka hapa nchini imepangwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu katika uwanja huo ambapo mara ya mwisho Simba na Yanga kukutana uwanjani hapo ilikuwa ni mwaka 2008.

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog amesema kuwa tayari ameshakiandaa kikosi kitakachovaana na Yanga ambacho anaamini kuwa kitaiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Katika mechi hiyo pia, Omog anatarajia kumuanzisha kiungo wake mkabaji na aliyekuwa nahodha wa timu hiyo msimu uliopita, Jonas Mkude kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar.

Omog amesema kuwa kiwango cha Mkude alichokionyesha katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1, kilikuwa cha juu hivyo kama atakuwa fiti zaidi anaweza kuanza dhidi ya Yanga akicheza sambamba na Mghana, James Kotei.

 “Kiwango alichoonyesha Mkude dhidi ya Mtibwa Sugar kulikuwa ni cha juu na alifanya kazi nzuri kama nilivyokuwa nimemwagiza.

“Endapo atendelea kuwa fiti basi kwenye mechi dhidi ya Yanga ninaweza kumwanzisha kama ilivyokuwa dhidi ya Mtibwa, kwani Yanga pia ina safu nzuri ya kiungo kwa hiyo kutokana na uwezo wake huo najua atawazidi ujanja hao akina Tshishimbi na Kamusoko,” alisema Omog.


Simba kwa sasa inaongoza msimamo ligi kuu ikiwa pointi 12 sawa na Yanga, Mtibwa Sugar pamoja na Azam FC lakini yenyewe ina mabao mengi ya kufunga kushinda timu hizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic