Gumzo leo ni nani atakuwa mchezaji bora wa dunia katika tuzo za Fifa kati ya Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa FC Barcelona.
Tayari wakali hao wawili wako ukumbini jijini London, England kwa ajili ya tuzo hizo za Fifa.
Messi na Ronaldo ambao ni washindani wakubwa wamekutana ukumbini hapo na kusalimiana.
Messi amewasili akiwa na mkewe Antonio Rucuzzo wakati Ronaldo alikuwa na mpenzi wake na mwanaye wa kwanza wa kiume.
Tayari mshambuliaji wa Arsenal, Olviere Giroud ameshinda tuzo ya Puskas ambayo hupewa aliyefunga bao bora na Kocha Bora amekuwa Zinedine Zidane wa Real Madrid.
0 COMMENTS:
Post a Comment