October 23, 2017


Mwigizaji Idriss Alba ameonekana si mtu mwenye mapozi wala kujivunga baada ya kuwafuata nyota, Lionel Messi, Neymar na Cristiano Ronaldo na kupiga nao picha kwa mtindo wa selfie.

Alba raia wa Marekani ambaye sasa anatamba na filamu ya Dark Tower alikwenda moja kwa moja na kupiga picha na Messi aliyekuwa amekaa na Neymar.


Baada ya hapo, akasonga na kupiga picha na Ronaldo aliyekaa karibu na mtoto wake wa kiume kwa mtindo huihuo wa selfie.

Wakali hao wako ukumbini jijini London kwa ajili ya tuzo za wachezaji bora za Fifa.

Messi na Ronaldo ndiyo washindani wakubwa na mmoja wao anatarajia kushinda tuzo hizo.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic