Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ameonyesha kufurahishwa na wachezaji wa Tanzania kuendelea kupata nafasi ya kucheza nje ya nchi.
Samatta ambaye anakipiga KRC Genk ya Ubelgiji, amesema wachezaji wengi kupata nafasi ya kucheza nje ya Tanzania inasaidia kuboresha ushindani nchini lakini kusaidia kuwa na kikosi imara zaidi cha taifa.
“Kuendelea kujiimarisha ni kuwa na njia sahihi tukianza kujenga misingi, lakini kabla tunaweza kuwa imara kwa kutumia njia hii ya kuwa na wachezaji wengi nye ya Tanzania.
“Ni jambo zuri ambalo linaweza kutusaidia kuwa na kikosi imara zaidi,” alisema Samatta.
Tokea ametua Genk, Samatta amekuwa akionyesha ushindani na sasa ni mmoja wa washambulizi hatari nchini Ubelgiji.
Mtanzania mwingine, Simon Msuva sasa anawika katika kikosi cha Difaa Al Jadid cha nchini Morocco wakati Abdi Banda ndiye beki tegemeo wa Baroka FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment