October 5, 2017



Pamoja na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba katika mechi ya kirafiki iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Kocha Mkuu wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo amesema wamefaidika.

Kihwelo maarufu kama Julio amesema wamefanikiwa kupata mafunzo na kujiimarisha.

“Tulicheza katika mpangilio mzuri kabisa. Tulikuwa tunajua kinachofanya na tuliwapana sana Simba.

“Lakini katika soka pale unapofanya kosa na mwingine analitumia mara moja lakini kwetu ni faida kubwa kwa kuwa tulicholenga ni maandalizi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Daraja la Kwanza,” alisema Julio.

Kikosi cha Dodoma FC kinashiriki Ligi Daraja la Kwanza na Julio amesema lengo lao ni kupanda ligi kuu.


1 COMMENTS:

  1. ww si ulisema umestaafu kufundisha soka sasa leo unasema umefaidika? kilichokuondoa mwadui na leo upo hapo dodoma ni nini? au ulidhani mtani atakupa ukatibu? uwe unajifunza kubaliza maneno wewe ni kocha mzuri lkn una maneno sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic