October 4, 2017



Beki wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda amesema atacheza katika klabu yake hiyo kwa mwaka mmoja tu.

Banda ambaye yuko nchini kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya kuivaa Malawi, amesema ana ndoto ya kufika mbali zaidi.

“Afrika Kusini sio mwisho, nataka kusonga zaidi nifike mbali. Nimepanga Baroka kucheza msimu mmoja tu lakini nimesaini miaka mitatu.

“Nataka nipate nafasi ya kwenda mbele zaidi, Afrika Kusini ni sehemu nzuri ya kupata nafasi ya kwenda mbele zaidi,” alisema.


Banda amejiunga na timu hiyo akitokea Simba na tayari amekuwa akionyesha kiwango kizuri akiwa na kikosi chake hicho cha baroka FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic