KIKOSI CHA YANGA MAZOEZINI KABLA YA KUANZA SAFARI YA KANDA YA ZIWA. |
Kambi ya mabingwa watetezi Yanga mjini Tabora iko vizuri na wanachotaka ni kumalizia kazi ya kuondoka na pointi sita Kanda ya Ziwa.
Yanga wameamua kuweka kambi mjini Tabora kabla ya kurejea mjini Shinyanga ambako watawavaa Stand United katika Stand United, wikiendi.
Mmoja wa maofisa wa Yanga amesema watajiandaa vizuri na kurekebisha mambo kadhaa ambayo wameyaona katika mechi ya dhidi ya Kagera Sugar.
Yanga iliitwanga Kagera Sugar kwa mabao 2-1 nyumbani kwake Kaitaba katika mechi ngumu ya kuvutia ya Ligi Kuu Bara.
Lakini Stand United wamekuwa wakitamba kwamba wataizuia Yanga na kuhakikisha haindoki na pointi mjini hapo.
Stand United wake mkiani wakiwa na point nne tu, juu ya Kagera Sugar na wanaonekana kutaka kujikwamua kutoka walipo.
0 COMMENTS:
Post a Comment