October 17, 2017


Kikosi cha Singida United, kimetua katika makao makuu ya wadhamini wake kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

Wachezaji, makocha na viongozi wa Singida United wakiongozwa na Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm wametua katika ofisi hizo zilizopo Oysterbay jijini Dar es Salaam kufanya ziara fupi.

Singida United wanakuwa wa pili kufanya ziara katika ofisi za SportPesa baada ya Simba ambao walifanya hivyo wiki iliyopita.


SportPesa kwa sasa ndiyo kampuni inayodhamini timu nyingi za Ligi Kuu Bara kwa wakati mmoja kwa kuwa inawadhamini Singida United, Simba na mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic