Beki wa zamani wa Simba, Emily Mugeta ambaye sasa anakipiga katika timu ya daraja la tano nchini Ujerumani, amefanyiwa upasuaji wa bega.
Mugeta ambaye aliwahi kucheza Simba akianzia timu ya vijana, amefanyiwa upasuaji huo leo.
“Bega lilinisumbua sana hata kabla sijaja timu hii, lakini mwisho nimepata matibabu na mwisho ni huu upasuaji. Nashukuru kila kitu kimeenda vizuri,” alisema Mugeta.
,
0 COMMENTS:
Post a Comment