November 16, 2017


Kiungo nyota wa zamani wa Manchester United, Eric Cantona ameonyesha kushangazwa na uamuzi wa Neymar kuhama Barcelona na kwenda kucheza soka nchini Ufaransa ambako amejiunga na PSG.

Neymar sasa ndiye mchezaji ghali zaidi duniani baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 198.

Cantona amesema anashangazwa na hilo kwa kuwa Neymar ndiyo ana umri wa miaka 25, vipi ahame Barcelona na kwenda Ufaransa ambako atashindana dhidi ya timu nyingi dhaifu.

“Kama ni ligi ya Mabingwa, huzo ni mechi chache tu. Zinaweza kuwa tisa, halafu basi. Baada ya hapo unashindana na timu gani unapokuwa katika ligi ambako ni mechi nyingi,” alisema Cantona na kuongeza.


“Kweli sielewi kabisa, vipi ameamua kuja kucheza huku Ufaransa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic