Mshambuliaji nyota wa zamani wa FC Barceloma, Samuel Eto’o amehusishwa na kuwaokoa Wacameroon waliokuwa wamekwama nchini Libya na kuelezwa wamekuwa wakiuzwa kama watumwa.
Imeelezwa kwamba Eto’o nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon kwamba amewalipia ndege.
Lakini kumekuwa na taarifa nyingine, kuwa atatoa fedha kwa kila Mcameroon aliyeokolewa.
Hata hivyo, Eto’o amekanusha suala hilo la kutoa fedha akisisitia upendo na hakusema chochote kuhusiana na yeye kuwaokoa au kuwalipia ndege.
Kumekuwa na taarifa ya wahamiaji hasa Waafrika weusi, kuuzwa kama watumwa katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ambayo imevurugika baada ya kuuwawa kwa aliyekuwa Rais wake wa muda mrefu, Muamar Ghadafi ambaye alikuwa kipenzi cha nchi nyingi za Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment