November 18, 2017




Kila mtu anakuwa na mawazo yake katika jambo fulani, lakini kiungo nyota wa Simba, Shiza Kichuya anaweza kutofautiana na wengi sana kuhusiana na Amissi Tambwe wa Yanga.

Kwa wale wanaoamini Tambwe anaweza kuibuka na kufanya maajabu na mwisho kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara, Kichuya anasema "haiwezekani hata kidogo."

Tambwe ni majeruhi ingawa tayari ameanza kufanya mazoezi mepesi na ligi inakwenda mechi ya 10 kwa kila timu katika mechi za leo na kesho.



Mshambuliaji huyo Mrundi hakuwahi kucheza hata mechi moja katika msimu huu na tayari aliwahi kuwa mfungaji bora mara mbili na mfungaji katika nafasi ya pili mara moja, hiyo ni katika misimu minne aliyocheza ligi hiyo.

Hadi sasa imeshapita michezo tisa ya ligi kuu huku wikiendi hii ikitarajiwa kupigwa kwa kumi, ambapo hadi sasa Tambwe hajafunga hata bao moja pia hajacheza hata mechi moja akiuguza jeraha la goti.


“Unajua kwa sasa ushindani umekuwa mkubwa sana kwa washambuliaji ambapo kila mmoja anakitolea macho kiatu cha ufungaji bora, kila mtu anajitahidi kufunga ili aweze kulifanikisha suala hilo.

“Ni ngumu kwa Tambwe kuwa mfungaji bora kwa sababu ameshakosa mechi tisa kwa sababu ya majeraha na hata akirejea haitakuwa rahisi kutukuta kwenye idadi hii ya mabao.

“Akirudi uwanjani, Tambwe atahitaji siku kadhaa za kurudisha makali yake sasa hapo na sisi tutakuwa tunapambana tufunge zaidi kwa hali hii naona haitakuwa rahisi awe mfungaji bora,” alisema Kichuya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic