November 15, 2017




Kampuni ya MultiChoice Tanzania imetangaza neema kwenye msimu huu wa sikukuu kwa kutoa ofa kabambe kwa wateja wake wa hapa nchini.

MultiChoice imetangaza neema hiyo leo kwa mteja mpya wa DStv ataweza kuunganisha kwa shilingi 79,000 ikiwa na vifaa vyote na kifurushi cha DStv Bomba cha mwezi mmoja.



Akizungumza kwenye Makao Makuu ya Kampuni hiyo Kinondoni, jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hilda Nakajumo alisema kuwa MultiChoice imekuwa na utamaduni wa miaka nenda rudi wa ikuwapa zawadi wateja wake wa Tanzania.

Nakajumo alisema, wateja wao wanapatia kila ifikapo msimu kama huu wa DStv kwa kuwatunuku wateja wake ili kuwawezesha kufurahia zaidi ya sikukuu.

Aliongeza kuwa, wanafahamu msimu huu wa sikukuu familia nyingi zinaungana katika kusherehekea, hivyo DStv imeamua kuwaongezea burudani kwa kutoa ofa hiyo kabambe.

“Tunapokuwa nyumbani na familia zetu, watoto wanataka waangalie katuni, sisi kinamama tunapenda kuangalia vipindi kama vile mapishi, urembo na tamthilia.

“Kinababa nao upend asana kutaszama michezo mbalimbali kama kandanda, hivyo kwa maana hiyo tumehamua kuwaletea burudani hii inayopatikana DStv,”alisema Nakajumo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic