| DK SHIKA AKIWA NA SALEHJEMBE ALIPOTEMBELEA OFISI ZA GLOBAL PUBLISHERS ZILIZOPO SINZA MORI JIJINI DAR RS SALAAM, LEO. |
Dk Louis Shika ambaye amekamata vichwa vya vyombo vya habari baada ya uamuzi wake wa kuzinunua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi, amesema anapenda michezo lakini si kihivyo sana.
Katika michezo anayoipenda, Dk Shika amesema kuwa anashabikia zaidi soka la England na timu inayomvutia ni Chelsea.
Shika ameiambia SALEHJEMBE kwamba anaupenda mpira na uamuzi wake wa kuishangilia Chelsea ni kwa kuwa inamilikiwa na rafiki yake.
Shika amesema Chelsea inamilikiwa na Roman Abramovich, bilionea raia wa Russia ambako Dk Shika alipata elimu yake ya udaktari.
“Napenda michezo na soka ndiyo zaidi. Timu za nje ndiyo napenda zaidi mpira wao, nashangilia sana Chelsea.
“Unajua mmilili wake (Abramovich) ni rafiki yangu,” alisema.







Heshima yake Dr. Louis Shika. Mmiliki wa kampuni ya Lancefort. Kama rais wa kampuni. Naamini unahtaj msaada wa kimataifa kukupa ulinzi wa kutosha.
ReplyDeleteWaliokuponda wataanza kukusalimia na wengne wataomba kazi ya ulinzi. Naamini hata tabasamu linaweza kukupa faraja.
Heshima yako tena