November 1, 2017



Unaweza kuona kwa muda mchache ambao washambuliaji wawili wa Yanga, Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa wamecheza pamoja, wameonekana kuelewana zaidi na kuwa tishio baada ya kukosekana kwa Donald Ngoma na Amissi Tambwe.

Ngoma na Tambwe ambao msimu huu walitarajiwa kuibeba zaidi timu hiyo kwenye safu ya ushambuliaji baada ya kuondoka kwa Simon Msuva, kwa bahati mbaya wameanza msimu vibaya kutokana na mara kwa mara kuwa majeruhi na kusababisha kukosa mechi kadhaa za Ligi Kuu Bara.

Kutokana na Ngoma na Tambwe kuwa wagonjwa, benchi la ufundi la Yanga chini ya Kocha George Lwandamina, liliamua kukomaa na kuijenga pacha ya Ajibu na Chirwa ambayo kwa muda mfupi imezaa matunda.

Katika mechi tatu za Ligi Kuu Bara zilizopita ambazo ni sawa na dakika 270, Ajibu na Chirwa ndiyo walianza kucheza pamoja kwenye nafasi ya ushambuliaji wa kati ambayo ni namba tisa na kumi na kufanikiwa kufunga mabao sita kati ya 11 ambayo timu hiyo imeyafunga mpaka sasa.

Wawili hao walianza kucheza pamoja dhidi ya Kagera Sugar ambapo kila mmoja alifunga bao moja kwenye ushindi wa 2-1.

Baada ya mchezo huo, wakakutana na Stand United na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0. Chirwa alifunga moja na Ajibu mawili.

Katika mchezo wa tatu ambao ulikuwa ni dhidi ya Simba, Chirwa alifunga bao moja kwenye sare ya 1-1. Kabla ya Chirwa hajafunga, Ajibu alimpa pasi Geoffrey Mwashiuya, ndipo akatoa pasi ya mwisho kwa mfungaji.


Wawili hao, wikiendi hii wanatarajiwa tena kuiongoza Yanga kucheza dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida katika muendelezo wa ligi kuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic