November 1, 2017



Inawezekana Msemaji wa Simba, Haji Manara akaingia matatizoni na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambalo limetaka ufafanuzi kutokana na kauli zake dhidi ya waamuzi waliochezesha mechi ya Yanga dhidi ya Simba.

Taarifa zinaeleza, tayari TFF wamesukuma barua kwenda Simba wakitaka ufafanuzi.

“Kuna barua imepelekwa kutaka kupata ufafanuzi kwa kuwa zinaonekana ni kauli za kichochezi,” kililieza chanzo.

Lakini mmoja wa maofisa wa Simba ameiambia SALEHJEMBE: “Hatujapokea barua yoyote, acha tuendelee kusubiri tutaona itakavyokuwa.”

Manara anatuhumiwa kuwashambulia waamuzi waliochezesha mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 na Yanga kuonyesha soka safi zaidi ya Simba hasa katika ushambulizi.

Lakini Manara alilalamika Simba kunyimwa penalti likiwemo lile tukio la Kelvin Yondani kuunawa mpira wakati akijaribu kuondosha hatari langoni mwake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic