December 10, 2017


Wapenda soka wengi nchini wameonekana kukerwa na kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichoshiriki michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya.

Hata hivyo, kero hiyo imezidi kuwa kubwa baada ya Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Ammi Ninje kusema “always next time”, akimaanisha wakati mwingine baada ya Stars kushindwa kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Leo mcha, Stars imefungwa kwa mabao 2-1 na Rwanda ikiwa imetangulia kufunga baadaye Amavubi wakasawazisha na kupata bao la ushindi.

Kili Stars inafungwa mechi ya pili mfululizo baada ya kuwa imelala kwa mabao 2-1 kutoka kwa Zanzibar Heroes ambao walianza kwa kufungwa, wakasawazisha na kupata ushindi.

Wakati akihojiwa, Ninje alionekana ni mchangamfu, akisifia vijana wake walivyocheza na kuongeza kwamba “until next time”.

Mashabiki wa soka wamekuwa wakijadili uwezo wake na baadhi wanaeleza kwamba Uingereza alifundisha timu za watoto na hakuwa na nafasi ya kufundisha timu ya taifa.


Wako ambao wanamtetea ambao ni idadi ndogo na kundi la tatu la mjadala ni lile linalowachambua wachezaji kutoonyesha juhudi.

7 COMMENTS:

  1. SI KILA KOCHA ANAFAA KUFUNDISHA TIMU YA TAIFA...:::
    Tusifanye vitu kwa kushinikiza...hii ndio inayotutokea puani sasa. Mimi naamini..si kila kocha anafaa kufundisha timu ya Taifa. Wapo makocha wataalamu kwa ajili ya Timu za Taifa.Nikwambie kitu...mbinu ya kocha wa timu ya Taifa ni tofauti na kocha wa vilabu. Kufeli kwa Maximo Yanga kulitokana na uzoefu wake wa kufundisha Timu za Taifa, kufeli kwa Van Gaal pia.

    Unapofundisha vilabu unajua nikikosa leo nitapata kesho ila timu ya taifa ukikosa leo umekosa kweli. Ninje si Mwalimu wa Timu ya Taifa. Hajui kupanga kutokana na uhalisia wa gemu husika. Tumekariri makocha na TFF yetu. Bado naamini tukiondoa uzandiki wa Uyanga na Usimba tutapata kocha na timu ya Taifa nzuri.

    Unaona Hemed Moroco na watoto wake???yule ni mzazi bhana..anajua jinsi ya kukaa na watoto wake na akawafanya waamini mihogo ni mikate na nyanya chungu (ngogwe) ni nyama....hawaingizi kichwani u--mlandege, u--miembeni wala U-JKU pale wanaenda kufanya kazi na kuonesha jamii kuwa ni Wazanzibar wale.

    Kila timu Tanzania inawachezaji zaidi ya 20 ambao ni wazawa kabisa. Vilabu vichace sana vina wachezaji ambao ni wageni hatuwezi kusema eti wageni wanachangia kuua timu yetu ya Taifa. Nikwambie..ukiondoa Strikers za wachezaji kutokea nje...ndani ya Nchi tuna strikers kali za Tanzania Prisons..tena ni Sumbufu kweli. Unakumbuka Yanga Vs Prisons (1-1)..unamkumbuka hata yule aliyempiga kiwiko Juma Abdul au yule aliyefunga Goal la Kwanza...basi hata Mohamed Rashid ambae ana goal Sita nyuma ya wachezaji wawili wa nje (Okwi na Chirwa)..ila yupo Striker wa Mbao ana Goli 6. Ila ukiacha hao wote...ukitaja strikers Halisi wa Kitanzania huwezi kumuacha John Bocco (adebayor)...Nimuite basi hata Waziri Junior. Unaijua beki ya Kati ya Mbeya City???mechi zidi ya Yanga hapa Dar aliumia na kutolewa ndio Yanga wakapata mwanya hata wakufunga. Wachezaji wapo ila sijui wanatoa tena percent ili wachaguliwe..???!!!maana kila siku na haohao. Hivi kwani Frank Dumayo kachoka sana???mbona Kenya namuona Black Berry anacheza. Sijaiangalia Uganda ila utakutaka na washikaji wa Chuji na Haruna Moshi kibao bado wanacheza. Huku kwetu magumashi sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sore braza, hapa mfano wa Van Gaal sijauelewa vizuri. Alifeli kwenye klabu au neshino tim? Asante.

      Delete
  2. Aibu, tena Aibu na inakera sana. Hii inamaanisha kama Zanzibar itapata uwanachama wa FIFA kuna uwezekano kabisa wa kutangulia kombe la Dunia wakiwaacha ndugu zao wa bara wakiendekeza misifa ya hovyo kwenye vyombo vya habari bila ya kwendana na sifa wanazopambwa kuwa wanazo. Tulitarajia mabadiliko baada ya kuingia uongozi mpya wa chama cha mpira lakini inaonekana kazi bado ipo. Watanzania wana tatizo moja kubwa la kukosa umakini na adabu katika kazi. Suala la kazi ya ukocha hasa wa mpira wa miguu si la kumjaribu mtu kama anaweza kwani vigezo na qualifications na uzowefu wao kwa madaraja husika ya ufundishaji kwa viwango vya timu mbali mbali hujulikana. Kuwa na cheti cha UEFA sio kigezo bora cha kukabidhiwa majukumu mazito kama ya timu ya Taifa? Kila mtu anajua kuchaguwa kocha wa timu ya Taifa sio jambo la kukurupuka. TFF ianaendelea kuboronga na itaendelea kufanya hivyo inaonekana hawana pressure na majukumu yao ya kazi hawakabiliwi na uchaguzi kwa hivi karibuni.Mkono wa serikali wa kuwaajibisha unaishia kwenye pazia la FIFA kwa hivyo watanzania wapenda soka tujiandae na machungu kwa kipindi kingine cha miaka minne. SISI watanzania ni watu wazembe sana mbona makocha wazuri duniani wamejaa tele tu. Kuna vibabu kule Ulaya vilivyolazimishwa kustaafu kufundisha mpira lakini bado wanauwezo wa kazi hasa katika nchi za Eastern Europe vimejaa ujuzi wa hali ya juu wanapatikana kwa bei poa na matokeo yake ni makubwa. Wale wazee ni wataalamu hasa na bado wanahamu ya kufanya kazi kutokana ukweli ni kwamba mpira haushi ushabiki licha yakuwa ni kazi. Unaweza ukampa ajira wazee kama wale kuwa kocha mkuu alafu ukamtafuta mzalendo kama huyu kocha alievurunda kule chalenji akawa msaidizi wake ili apate uzowefu. Kwa kawaida ya watanzania mtu akijua kufungua vioo vya gari atakwambia yeye anauwezo wa kurusha ndege.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakubaliana makocha bora wako ktk nchi za kutoka EASTERN EUROPE na PIA NERTHLAND.
      Namkumbuka sana kocha VICTOR STANSLECUS toka Rumania akifundisha YANGA ktk miaka ya mwisho 1968-1972 na jinsi alivyoibua Yanga kids ya kina Pondamali, Adolf.Kuna sasa kocha mrumania wa AZAM na unaiona team imeanza kucheza la kitabuni.Angalia national team ya Rwanda au Uganda chini ya MICHO tokea SERBIA.Angalia Simba ilivyokuwa chini ya CIRCOVIC naye tokea SERBIA.
      Kuna makocha wazuri wengi kutoka ktk nchi za Eastern Europe na binafsi nawakubali na isitoshe chenji yao is reasonable.

      Delete
  3. Tanzania sijui tumerogwa??? Yaani sielewi. Labda tubadili jina liitwe lile la zamani la Tanganyika pengine kuna kitu tumekosea.

    ReplyDelete
  4. mie naomba niwe na mtazamo wa TOfauti kidogo na wengi, tusikimbilie kulaumu tu juu ya matokea haya, sote twajua kuwa kocha mpya na kachagua team mpya akiwa na falsafa mpya, ni rahisi kurusha lawama ingekuwa ni Mayanja lakini kwa Ninje hali ni tofauti kidogo maana ndio anaichukua team mara ya kwanza, anaanza na wachezaji wapya kabisa na kwa kikosi ambacho ni kipya pia

    ReplyDelete
  5. Masuala ya kumjaribu mtu katika kazi yenye majukumu mazito sio sahihi wakati watu wenye uwezo wa kazi wapo. Binafsi mimi naona sio sawa kumlaumu kocha na kuwaacha wahusika wakuu waliompa ile kzai wakipeta. Watanzania ni watu wavumilivu sana na walishavumilia vya kutosha mauzi ya timu yao ya taifa lakini wahusika ama hawajui wanachokifanya au hawajali timu yetu ya Taifa kuendelea kuwa kichwa cha mwenadawazimu. Mfano mzuri tu ni katika maamuzi magumu waliyofanya CCM kumsimamisha Magufuli kugombea uraisi . Magufuli hakusimamishwa kugombea uraisi kwa sababu ni Msomi mzuri mwenye shahada ya PhD nakadhalika la hasha. Kilichopelekea Magufuli kupendekezwa kuwa raisi ni vigezo na matokeo katika utendaji wake wa kazi. Kama kuna kitu Watanzania walipatia katika historia ya nchi yetu basi ni uteuzi wa Magufuli. Na hii inaonesha yakwamba bado tukiamua watanzania tunaouwezo wa kufanya mabadiliko ya maana katika taasisi zetu za umma. Kocha wa timu ya Taifa sio wa TFF ni kocha wa watanzania sio sahihi hata kidogo kulichukulia jambo hilo kuwa ni jambo la mzaha hata kidogo na maamuzi yeyote juu ya uteuzi wake lazima iwashirikishe wadau mbali mbali ili kumpata mtu sahihi .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic