Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yaingiwa na hofu kwa kiwango bora wanachoonyesha timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) katika Mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup yanayoendelea nchini Kenya.
Hofu hiyo imekuja jioni ya leo katika uwanja wa Kenyatta Mjini Machakos mara baada ya kutoka sare ya 0-0 na Wenyeji Kenya na kupelekea Zanzibar kutinga moja kwa moja nusu fainali wakiwa na alama 7 wakiongoza kundi lao A lenye Mataifa kama Kenya, Libya, Rwanda na kaka zao Tanzania bara.
Baadhi ya wajumbe wa CECAFA wakiongozana na wakaguzi wanaopinga dawa za kuongeza nguvu Michezoni walikwenda kwenye vyumba vya kubadilisha nguo vya Zanzibar Heroes kwa kusema haiwezekani timu ya Zanzibar icheze michezo mitatu mfululizo bila ya kuonekana kuchoka.
“Mechi tatu mfululizo Zanzibar wanacheza kwa kiwango bora, tena wachezaji wao ndo wale wale kila siku wanaoanza labda abadilike mmoja tu, itakuwa wanatumia dawa za kuongeza nguvu lazima wachunguzwe”. Alisema mmoja wa Afisa.
Uongozi wa Zanzibar Heroes ukakubali wachezaji wake kwenda kupimwa kama kweli wanatumia dawa za kuongeza nguvu au kiwango chao tu,ukatokea mtafaruku baina yao wenyewe viongozi wa CECAFA na mwisho wakakubali kuwaachia wachezaji hao waende zao wachezaji ambao walishangazwa mno kusikia kuwa wanatumia dawa.
KUNYA KANYA KUKU....AKINYA BATA...!!!
ReplyDeleteHuu ni msemo wa watu wa kale waliokuwa na miono ya maelekezo ya kimaisha kwa kutumia lugha malidhawa ya Kiswahili. "USIIGE TEMBO..."" ni maneno magumu ambayo katika lugha rahisi linaleta maana tofauti. Unajiuliza "Je wazee wa kale walikuwa hawaogopi matusi??"..la hasha hii ni lugha tu..na maneno yote yanatumika katika lugha.
Hivi ndivyo ninavyoweza kufananisha na Timu ya Zanzibar...leo wao ni bata. Wangekuwa kuku wangeonekana ni kawaida yao. Wataalam wansema "AKILI ZA KUPEWA CHANGANYA NA ZAKO"..siamini kama walienda kuwakagua wachezaji wote kama wanatumia dawa za kuongeza nguvu kwa kuwa kila mashindano yana utaratibu wake. Mchezaji kuchukuliwa kama sample ya ufanisi wa upimaji huwa sio tatizo.
Shida ninayopata ni kwamba Zanzibar ya akina Selembe, Muda, Ahmada, Karie, Mwinyi...imekuja na mapinduzi ya kiufanisi. Usisubili mtoto wako amalize shule ndio umpe hongera kwa mazuri yake..basi hata pale anapojitahidi darasani mpe hongera yake. Mi naanza kabisa hata mkitolewa leo "HONGERA ZENU"...kuna kitu wana-improve katika mfumo wa soka Tanzania.
Ujuaji mwingi....nyuma giza..hii ni sentensi nyingine inayopendwa kusemwa na wale wanaowaona watu wanaojifanya kujua sana alafu hakuna kitu. Usikatae kushikwa mkono na kuvushwa barabara kama ulitoka siku nyingi Dar es Salaam..utagongwa na Mabasi ya Mwendo kasi. Tukubali ushamba wetu utaturudisha nyuma. Tusijifanye wajuaji sana wakati Mjomba angu Morocco anatushinda. Na usikubali kupewa majukumu kama huyawezi.
DARASA ALISEMA "tuache maneno tuweke muziki"...tuache maneno tufanye kazi. Kila mtu awajibike. Mchambuzi usiwe kocha na kocha usiwe mkurugenzi.
TUFANYE KAZI