December 12, 2017Uongozi wa klabu ya Simba ililazimika kufanya umafia na kuyamaliza mambo kimyakimya huku watu au mashabiki wake wakiendelea kuwa na hofu.

Wakati mkataba wa beki wake Juuko Murshid ukienda ukingoni, Simba ilimuita mezani na kumsainisha mkataba wa miaka miwili fasta.

Pamoja na kufanya  hivyo ukaendelea kukaa kimya bila ya kueleza jambo na hivyo kuwafanya watani wake Yanga kuendelea kumfuatilia wakitaka kuimarisha kikosi chake katika safu ya ulinzi.

Hata hivyo, Yanga imekuja kushituka mwishoni kwamba Simba ilishamaliza mchezo na kukaa kimya kabisa.

Kwa sasa, Juuko anaitumikia The Cranes katika michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya.1 COMMENTS:

  1. Huyu Kichaka tu cha Obray Chirwa. Atakatiza hapo faster akiwa na Ajibu wa mguu wa Dhahabu.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV